KIFO NA HUKUMU YA MWISHO (ZAB 146:3-4) • Siku za mwanadamu ni chache kama majani isaya 40:6-8,job 14:1-2,1 pet 1:24-25. • Mwanadamu ni msafiri na mpitaji.1Pet 2:11,,, • Mtu ni kama mchanga na mvuke yakobo 4:13-15,Mwanzo 3:19, (kwa hivyo mwanadamu asijivune wala kuhangaikia Maisha.Yakobo 4;13. • Mtu akishakufa hawezi kurudi kwake wala kuona mema ayubu 7:1-10,2 Samueli 12:22-23 • Mwanzo wa kufa-Mwanzo 3:19. • Aliye kufa ni mali ya Bwana –Warumi 14:8, mwanzo50:1 lakini mkristo asilie kama watu na mataifa 1 thes 4:13-18. • Wakati mwingine usijihusishe sana na mambo ya mazishi ikiwa yanagongana na huduma ya neno mt 8:22. • Yule hajaokoka pia amekufa kiroho -1 Tim 5:6,kolosai 2:3,Rom 6:11. • Babu zetu walisafirisha maiti na si vibaya kusafirisha maiti leoila si lazima sisi tufanye hivyo, mwanzo50:4-7,25,Kutoka 13:19. • Tuachane na mila zinazo husu mtu aliye kufa -1 Thes 4:16,1 kor15:21- • Maiti(mwili ambao ametokwa na uhai) haujui chochote –ayub7:5-10,Mhubiri 9:5. • Maiti (mwili ambao imetokwa na uhai) hawezi kurudi nyumbani kwake-Ayubu 7: 5-10. • Si lazima maiti azikwe na umati mkubwa wa watu-matendo 5:6, Luka23:50-53. • Mababu walikuwa na mahali pa mazishi (makaburi)-mwanzo 23:10-9. • Maiti huzikwa –matendo 5:6,kumbu34:6, mwanzo 23:10-19. • Vitabu vingine juu ya kifo ni Mhubiri 6:12,1thes 4:13-18,Mwanzo 3:16,1 kor15:12-57,Ufunuo 14:13,30:23,1 pet 1:24,zab 116:15,102:3-4,90:3-10,39:5-10,Yakobo 4:13-14 • Ni afadhali kuiendea nyumba iliyo na matanga.Warumi 12:15,Mhubiri 7:2,4 • Kula dhabihu zilizotolewa kwa wafu ni dhambi zab 106:28, ufu 2:14, hes 25:1-13, kut 34:15, 1 kor 8:10, 10:20-21 Mtu akifa anaenda wapi? Kuna sehemu mbili tofauti ambazo wanaokufa wanaenda kukaa wakingoja kufufuka kwao na hukumu ya mwisho. Kulingana na matendo yao ufunuo 14:13-14 Sehemu hizo ni: 1. Watakatifu kuwa pamoja na Yesu. 2. kuzimu Watakatifu kuwa pamoja na Yesu. Mungu anafurahia mtu kufa akiwa mwenye haki Zab 116:15. Katika agano la kale watakatifu walipokufa malaika aliwapeleka kwa kifua cha Ibrahim, Luka 16: 22-23 mahali ambapo katika Agano Jipya panaitwa kuwa pamoja na Kristo Wafilipi 1: 20–23; 2Kor. 5: 8. Luka 23: 43, na siku ya hukumu ya mwisho, hawa watakatifu wataishi Yerusalemu mpya milele. Ufunuo 21: 1-5. anayekufa akiwa ameokolewa anaingia katika uzima wa milele,Mt 25:34,Ufunuo 14:1 Watakatifu ni wale wanaoamwamini Yesu na wanatii neno la Mungu.Mt 7:24-26,Yoh 15:1,10,14,8:30-32,Isaya 66:2, Yesu hakubaki kuzimu, ila alichukuwa Funguo za kuzimu, Ufunuo 1:18; Matendo 2:27, luka 23:43 Kanisa linashinda Milango ya kuzimu. Mt. 16:18; Yesu alienda kuwandalia makao mazuri, Yohana 14:1-2; Ufunuo 21:1-5; 22:1-5 KUZIMU: Isaya 14:9-15, Mithali 7: 27, Luka 16: 19-31. Kuzimu ni mahali ambapo watu wanaokufa wakiwa ndani ya dhambi huenda,kukaa vifungoni kwa mateso wakingoja kutupwa kwa ziwa la moto siku ya hukumu.2 wathes 1:4-20, Lk. 16: 23; Mat. 11: 23; Mrk 9: 43-46 Mithali 27:20,32:16, Luka 16:25 Yohana 5:28,29 Mt 22:13,25:41,Ufunuo 21:8.Na Yule Mt 5:22, Mt 10:28, 8:8-10, Lk 12:5 . kuzimu kuna sehemu inayoitwa giza la nje, hapa ni mahali ambapo wana wa Ufalme wanaoasi(wanafiki) watatupwa, ni mahali pa kulia na kusaga meno Mat. 22:13; 8:12; 24:51 jehanam ilitengenezwa kwa ajili ya shetani na Malaika zake, lakini watu wanaotenda dhambi wanaenda kukaa na shetani kwa huo moto milele na milele -Zaburi 9:17 Mithali 7:27,9:18,ISaya 19:12,5:14,34:9,Mariko9;43-48 waebrania 10:26-27,20:12, 22:19,Wagalatia5:19-21, luka 16:9-35,,12:51,mt,23:33,5:22;10,22,10;28. Yesu alipokufa alienda kuzimu akahubiri injili ya neema na kuchukuwa funguo za kuzimu, na hata leo hii bado Yesu ana uwezo wa kuingia na hawezi kukwama huko. 1Pet.3:18-21, 1 Pet 4: 6; Ufunuo 1: 8; Matendo 2: 27 Mifano ya wale wako kuzimu. ( Mahali pa kulia na kusaga meno Ufunuo 14:10-11, Kumbu 32:22, Mark 9:43-48, LK- 12:5, Mt 10:28(Mungu hapendezwi na kifo cha wenye dhambi Ezekiel 18:23) 1. Wanao mwamini Yesu lakini wanaendelea kuishi maisha ya dhambi wakifa wanaenda kuzimu Wagalatia 5:16-19, Mt 22:13, 8:11-12s. 2. Wasioamini Yesu wakifa wanaenda kuzimu., Yoh 3: 18; Zab. 9: 17; Mt. 11: 23Mungu yuko kila mahali, Methali 15: 11; Zab. 139: 7. 3. Malaika walioasi wako vifungoni kuzimu 2Peter 2:4; Yuda 6 inasemakuwa mapepo mengine yatafunguliwa wakati wa mwisho. Ufunuo 9:1-11. 4. Miji zizisoitikia mwito wa toba zitatupwa kuzimu, Mat. 11:23Tajiri alikuwa kuzimu, Luka 16:23 5. Wale wasio mwamini Yesu Kristo kuwa mwokozi wanaenda motoni ikiwa watakufa kabla ya kumwamini Yesu kuwa mwokozi wao-Yoh 3:16-17. 6. Wale wanao mwamini Yesu Kristo kuwa mwokozi wa maisha yao na kujua neno la Mungu lakini hawajatii hilo neno la mungu (injili) ila wanaishi maisha ya dhambi wanaenda motoni- wasipobadilika -2 wathesalonika 1:6-8,Ebr 10:26-27,Luka 12:47-6:46-49,mt 7:21-26. 7. Wale waliomwamini Yesu Kristo na baadaye wakarudi nyuma wanaenda motoni wasipo mrudia mungu tena.2Pet2:20-22,Waebrania10:35-39. 8. Viogozi wa kanisa ambao wamebadilisha neno la mungu kuwa biashara yao na kutoa ili kupongezwa (harambee) .Wanaohubiri kwa ajili ya mshahara tu wakiambia watu watoe pesa au vitu ndipo waombewe na kuhubiriwa jinsi ya kutajirika au kutafuta mali ya dunia pekee. wanaenda motoni wasipo tubu Yakobo 5:1-4, 1 Tim 6:1-10, Mariko 10:17-26 9. Viongozi wakanisa na watu wengine wanaopanga au wanao wasaidia washiriki kupanga / kutimiza mila au utamaduni kama makumbusho ,teroburu, tohara za kienyeji ambazo ndani yake vijana ufundishwa uchawi ,na tohara kwa wasichana, mila ya kufanya ngono kabla ya kupanda mbegu , kulala na maiti, wote wanaenda motoni wasipobadilika Mariko 7:1-9Wakolosai2:8 Waefeso4:22 Zab 106:28. 10. Wote wanaoleta mitindo ya ulimwengu kanisani ambao wakija kanisani wanacheza miziki ya kitamaduni na kufanya harambee iliyo na mizaha, matani,ubishi wakati wa matoleo, na wanawake wanao timiza tamaa ya mwili na tamaa ya macho na kiburi cha maisha (1 Yohana 2:15-17) kupitia kwa kujipamba kwa nje tu kama makahaba kupitia mitindo yakushuka nywele zao, kuvaa vipuli, kutumia marashi, kuvaa mavazi mafupi au yanayoacha miili yao uchi au wanawake wanao vaa mavazi yanayostahili kuvaliwa na wanaume lakini wakaacha kupamba mioyo yao kwa kuwa watakatifu wasipotubu wanaenda motoni mwanzo 35:2-5, kutoka 32:1-3, 33:4-6, kumbu 22:5, isaya 3:16-24, 1pet 3:3-4, 1tim 2:9 11. Wanasiasa na mashabiki wao wanaokwenda kwa waganga ili kupata umaarufu na kutumia jukwaa zao kwa matusi na pia wakija kanisani ili kuombewa na wana ahidi watu ahadi nyingi za uongo huku wakichochea watu kupigana na kuchukiana na kuchochea ukabila wanaenda motoni wasipobadilika Wakolosai 3:5-11, Isaya 8:19-20,Mambo ya Walawi 19:31 Kumbukumbu 18:10-13 12. . Mazoezi ni mazuri kidogo (1Tim 4:8) lakini wakristo pamoja na watu wengine wakiingia mazoezi kama za mbio, kucheza mpira, kuruka ,michezo za kuchekesha watu na wakasahau kuangalia utakatifu badala yake wakaenda kwa waganga ili washinde au wakawa na michezo inayoleta mizaha ,matani, ubishi ,maringo kiburi kutumia madawa ya kulevya na bangi ,kupigana na matusi na kuwaadhimisha wachezaji- wako njiani kuenda motoni wasipotubu- Wagalatia 5:19-21, Zab1:1Kor 15:33, 6:9-10 9). Mzee anayemwacha mkewe na kumwoa mke mwengine pamoja na na mke anayemwacha mumewe na kuolewa na mume mwengine ni wazinzi, Kwa hivyo wanaenda motoni – luka 16:18,,1 Kor 7:10-11,Warumi 7;2-3, Mariko 10:2-12, 1 Kor 7:10 13. Wale walio ndani ya madhehebu ambayo yamekataa kutii neno la Mungu ambayo yanafanya vitu kwa njia tofauti na vile biblia inasema kwa mfano badala ya kubatiza waumini ndani ya maji mengi, wao wanapaka wakristo mafuta au kuwa simamisha chini ya bandera au kuwafanya waruke juu ya moto wakiita hizo vituko kuwa ni ubatizo na pia viongozi wao hupenda kufanya vitu ili kutazamwa na watu na kupongezwa na watu wote wasipobadika wako kwa njia ya kuelekea jehanamu (motoni)Mathayo 7:13-27, 6:1-4, 23:1-16, Yakobo 2:1-9, Luka 14:7-14 14. Mashoga, washerati, wenye kusengenya, wazinzi, wachoyo, wasingiziaji, wasiosamehe, wasiopenda, wasiotii wazazi katika Bwana, walio ndani vyama vinayoitwa vya maendeleo lakini vina sheria zilizo kinyume na biblia; wale wasiojali wajane na mayatima na wasiojiweza na wengine wote watendao maovu hayo wanaenda motoni wasipo tubu- Wakolosai 3:5-10, Warumi 1:23-32, 2 Tim 3:1-6, 1Yoh 3:15, 14. Mark 11:26, Mt 25:41-46, Yakobo 1:27. Isaya 1:17 15. Wafanya biashara na wakulima wanaolima na kuuza bangi,tumbako wale wanaotengeneza sigara na kuuza pombe na walevi na wale wanaofanya kazi kwa kampuni za kutengeneza Pombe na wafanya biashara ,wanaotumia hongo ujanja ,unyangaji , wizi, na wale wanao tumia madawa za waganga kuendesha biashara yao na wale wanaonyang’anya watu mashamba na vitu vingine walivyowauzia, wale wanapora mali ya wengine,na wale hawalipi wafanyi kazi pamoja na wafanya kazi ambao hawafanyi kazi yao kwa uaminifu wote wako njiani kuenda motoni wasipobadilika- Yakobo 5:1-4 Mithali,23:29-30,Habakuk 2:15,Wakolosai3:5-9 Isaya 5:21-22, Amosi 8:4-8, Mika 6:10-11, Yeremia 5:27-28 Siku Ya Hukumu mt25:31-46, ufunuo20:11 Ukifika wakati wa hukumu ya mwisho, kuzimu itapeana wafu walio ndani yake ili watupwe kwenye ziwa la moto, Ufunuo 20:13. Kuzimu itatupwa kwenye ziwa la moto, Ufunuo 20:14 Lile mtu afanye ili kuepuka jehanam Kukosa kutii kile mungu anasema nis dhambi..Adam na Hawa walipotenda dhambi,wanadamu wote wamehesabika kuwa wenye dhambi tangia tumbo la mama yao-Warumi 3:23,Zaburi 51:5. Mshahara ya dhambi ni mauti Warumi 6:23 ila tunapomwamini Yesu Kristo na kutii neno lake tunasamehewa dhambi zetu zote -Warumi 3:24,25.Wale mbao wanajitahidi kutenda matendo mazuri bila kumwamini Yesu Kristo badu wako na dhambi zao. Lazima tumwamini Yesu kwanza ndipo tuhesabiwe haki bure kisha tuendelee kutenda matendo mazuri .Yoh 3:16-20.Inawezekana kuna vitu ambavyo tunafanya sisi wenyewe bila kujua kuwa ni dhambi na hiyo haibadilishi hizo vitu kuwa vizuri na ndiyo sababu kila mara tunafaa kunyenyekea kwa mungu ili kwa uwezo wa Roho mtakatifu, tufunuliwe juu ya dhambi na tudumu katika kutubu na kutafuta kutakaswa na kusamehewa hata na dhambi ambazo hatujui tunapozifanya.Mambo ya Walawi 5:15-17,Zaburi 19:12,Luka 12:48,Yohana 1:6-10,na pamoja na hayo,tujitahidi kujilinda ili shetani asituingize kwa dhambi-1Yohana 3:2-10.Baada ya kumwamini Yesu,haifai tuendelee kutenda dhambi kusudi baada ya kujuwa ukweli-1Kor 5:9-13 Waibrania 10:24-39 1kor 5:16-18,Wahibrania 6:1-10 2Pet2:20-22 ila tunafaa kuchukia dhambi na kuziacha –1Pet 1:13-15,1Petro 4:1-4 Waefeso 4:22-23 1Pet 3:9-11, 1Yohana3:24 1Yohana 2:29 , kwa wale wanaogafulika katika kufanya dhambi-bila wao wenyewe kupenda wasaidiwe kwa upendo kwa kumrudia Mungu, tusifuraie na kuchekelea na kuhukumu wakati mkristo amerudi dhambini-Yakobo 5;19-20,Wagalatia 6:1 1yohana 2:1-2 mt7:1-2, Luka 15:21-27, kumbuka Mungu alimsamehe Daudi dhambi aliposhauriwa kutubu-2Samuel 12:13,Zaburi 51:1-