UPENDO
1 yohana 2,3,4,5,1 wakorinthon 13-14;1
Musa alileta amri kumi lakini Yesu alikuja na amri moja mpya ambayo ni upendo yohana 15:12,yohana 13:34.Ukiwa na upendo,una amri zote za Yesu Kristo.Yesu ni upendo 1 yohana 4:7-8,5:2.Kwa hivyo,ukitaka kuwa na upendo,mpokee Yesu moyoni mwako nawe utakuwa umepata upendof,ndipo unakuwa mkristo kamili naye anatii kila neno lililonenwa na Yesu kristo.Yohana15:3,10,14,Yohana 14:15,Mt 7:24-26.Ikiwa hauna upendo,inamaanisha kuwa hauna Yesu ambaye ni upendo na bila upendo,mambo yote unayofanya si sawa.1wakorintho 13:1-3,14:1.Kila mkristo anafaa kumpenda Mungu na Mwanadamu.
Jinsi ya kumpenda Mungu Luka 10:27
Unampenda Mungu kupitia kutii neno lake.1yohana 5:3,Yohana 15:3,10,14.Yohana 13:14,Mt 7:24-26.
Jinsi ya kumpenda mwanadamu
Ili kumpenda mwanadamu,unafaa kufanya mambo haya:
Jua kuwa Mungu ni upendo 1 Yoh 4:7-8
Jua kuwa Mungu alikupenda kabla umpende 1Yoh 3:16-17,Yohana 3:16
Mpokee Yesu ambaye ni upendo.Yohana 15:4
Muone Yesu ndani ya wanadamu wengine .Mt 25;31-40,
Jua kuwa yote unayomfanyia mwanadamu unamfanyia Yesu.Wakolosai 3:23,Mt 25;40
Jitolee uhai wako kwa ajili yaw engine.1Yoh 3:16,17.4:11
Anza kufanyia watu vitu ungependa wakufanyie.Luka 6:31
Anza kuwaona watu wengine kuwa bora kuliko wewe.Wafilipi 2:3-4
Usiuzuie msaada wako kwa watu kama una uwezo wa kuwasaidia.Mithali 3:27-28.Ujue kuwa watu wote walemavu ,waliorukwa akili na wote wasio na kitu ni watu wa Mungu na pia ujue kuwa Mungu alikuona ukiwa na akili nzuri na nakakupa mali yako na ya mtu asiye na akili nzuri au maskini na mlemavu ili umtunzie,kwa kuwa huyo angepewa mali,angeiharibu na haingemfaidi kwa muda unaofaa,hivyo Mungu alikupa mali yako nay a huyo mwengine ili uwe kama mlinzi.Kila mara unamuona mtu anakuomba msaada mpee kwa sababu Mungu alikuweka umtunzie .
Usimchukie mtu na huku unasema kuwa unampenda Mungu[ 1yoh 4:19-20] [luka 6: 27-36 ] [warumi 12: 14-20]
Ili kupenda lazima uwe mtu wa kusamehe na kutolipa baya kwa baya [mrk 11:25-26]mt6;12,14 warumi12;14-20,mt 5:21-26 ,waibrania 13:1-2,luka 17:3-4,
Anza kusaidia watu wote wazuri na wabaya Mt 5:43-45 ,luka 6:27-36,
-Wasaidie Mayatima na wajane yakobo 1:27, 1tim 5:3-11 wala usiende kuridhi mjane na lengo ya kuharibu mali aliyo achiwa na mume wake Mt 23:14
– Wasaidie walemavu, vipofu na maskini luka 14:12-13 ,3:11. [Waandalie karamu, wanunulie mavazi na uwape chakula ]. Ikiwa unaishi na mlemavu au yatima au mjane au maskini yeyote usimtumie kwa ajili yako kufaidika bila kuangalia kile ambacho anapata kwako . Ukiishi na maskini , yatima , mjane au mototo wa mtu mwingine mhudumie jinsi unahudumia watu wa familia yako wala usipendelee yakobo 2:1-17
– Wasaidie hata watu ambao hauwajui luka 10:25-37
– Wafadhili wageni waibrania 13:2
-Wasaidie watu kutoka makabila mengine luke 10;27-37
-Hudumia / Tembelea wagonjwa yakobo 5:14-16 Mt 25:31-40 kuna wale hawasaidii au kutembelea mtu akiwa mgonjwa lakini wakisikia kuwa huyo mgonjwa amekufa wanakimbia huko na kujitolea kununua jeneza nzuri na nguo mbayo maiti atavalishwa lakini alipokuwa mgonjwa hawakumsaidia ilia pone hayo ni makosa .Madhehebu mengi yana hazina ya ujenzi na kifo na mazishi lakini hawana hazina ya kuwasaidia wagonjwa ,mayatima, walemavu na wajane hayo ni makosa.
Kopesha watu luka 6:32-36 ,lipa deni warumi13:8 zab 37:21 -Ukiwa na wafanya kazi watendee haki , walipe mshahara wao na uwafanyishe kazi kwa kiasi kinachofaa ukiwaruhusu kwenda kanisani, kutembelea watu wa ukoo pamoja na marafiki ,yakobo5:1-6
-Ukiomba kitu cha mtu mrudishie na usingoje aje kufufuata mwenyewe na usidhulumu watu wala usimnyang’anye mtu shamba au kitu ulichomuuzia ,na usiue kwa sababu haya maovu yana matokeo mabaya [habakuki2:9-12 yeremia 5:27-29 Amos 5:11-12 mika 3:10,6:10-15 ,mwazo 4 :10-12 ,mithali 3:10-11] Toba yasawa kama umemnyanganya mtu kitu nikumrudishia luka 19:8 Isaya 58:
Penda jirani
Kulingana na Yesu,jirani ni yeyote unayekutana naye
katika safari ya maisha-Lk 10:30-37
Mifano ya jirani ni: Familia ,marafiki,maadui,wageni n.k
i)Penda Familia yako
Ni muhimu kwako kuomba na kutakia familia yako kuokolewa wote-Matendo 16:31:34, Yoshua 24:15
Penda ndoa yako-mume na mke wafanye mambo yao yote pamoja-Mrk 10:6-9
Mungu amekataa talaka- 1Kor 7:10-11,Mrk 10:1110:11-12
Heshimu ndoa –Ebr 13:4
Mungu amekataa usherati-1Kor 7:2
(2)Marafiki zab 27;17/mathayo 17;17
Uwe mwangalifu katika kuchagua marafiki_Zab 119:63
Kuteseka kwa sababu ya rafiki_Yoh 15;13
(3)Maadui mt 5:43_48
Penda adui
Ombea adui ili Mungu ampe kupenda
Usilipishe mabaya_warumu 12:17_21
Usikasirikie adui_wakolosai 3:13
Upigane na shetani aliye ndani ya adui kwa maombi_waefeso 6:10-13
Ikiwa ni wewe ndiye unasababisha jirani kukuchukia,tengeneza uhusiano.
Unaweza kuchukiwa kwa sababu ya wokovu ila uwasamehe na uwaombee na usiwachukie wale wanaokuchukia_mt 7:58-60, Lk 23:34 Yoh 15:18-21,16:1-2,Mt 10:34-37
matokeo ya kusaidia watu
Unapowasaidia wanyonge unamkopesha Mungu naye atalipa Mithali 19;17 na unapokosa kusaidia wanyonge na wewepia utakosa msaada Mithali 28:10 ,26: 27 Warumi 12:17
MATUNDA MENGINE YA UPENDO [ 1 Wakor 13:1
Upendo huvumilia – Ukiwa na upendo utavumilia hali zote ndani ya wokovu
Upendo hufadhili- ukiwa na upendo utasaidia watu
Upendo haujivuni-ukiwa na upendo hautajivuna
Upendo hautafuti mambo yake- ukiwa na upendo unatafuta ufanisi wa wengine
Upendo hauhesabu mabaya – ukiwa na upendo unafunika ubaya 1pet 4:8, unaendelea hata kusaidia hata adui yako
Upendo haufurahii udhalimu –ukiwa na upendo hautafurahia mizaha, matani,ubishi au kuona mtu anatenda dhambi bali utawahubiria ukweli
2Kor 2:5-11)
Kiongozi wa kanisa akilikosea kanisa.1Timotheo 5:19-20,
Mzushi anayelikosea kanisa .Tito 3:10
Adui wako ,Mathayo 5:43-45,Luka 6:27,Warumi 12;14,17-20,
Utasamehe kina nani?
Yesu alitusamehe
Baba ,mama awasamehe watoto, kwa mfano,kijana mpotevu alisamehewa.Luka 15:11.
Watoto wasamehe wazazi wao na ndugu zao.Kwa mfano Yusufu .Manzo 45:15,50:15-21.
Majirani wasameheane
Uwasamehe maadui zako,kwa mfano,Stefano aliwaombea msamaha waliomwua.Matendo 7:59-60
Yesu aliwaombea waliomuua msamaha.Luka 23;34
Watu wa familia wasameheane.
Mwajiri na mfanyakazi wasameheane.
Ili kuonyesha umesamehe mtu,endelea kumsaidia ,ogea naye,msalimie na usilipize kisasi.Luka 6;27,Warumi 12:14,17-20, 1Wathesolanike 5:15,.,pia ujifanye kama usiyeona makosa unayotendewa.Mithali 19;11.
Unkimfanyia adui yako mema,naye anaendelea kukutendea mabaya,matendo yako mema kwake yanabadilika kuwa makaa ya moto juu ya kichwa chake.Warumi 12:17-20 na pia mitego anayokuwekea ,mwenyewe huanguka ndani..Mithali 26:27,Esta 5:13,7:9